Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Sanandaj Iran, kikao maalumu kuhusu nafasi ya walimu wa hawza na vyuo vikuu katika diplomasia ya kielimu kilifanyika katika Chuo Kikuu Huria cha Kurdistan, kwa hotuba ya Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Mofid Hosseini Kouhsari, Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza za Kielimu nchini Iran.
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza, akielezea umuhimu na ulazima wa diplomasia ya kielimu kama moja ya vipengele vya nguvu laini ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran—hasa baada ya vita vya kulazimishwa vya hivi karibuni vya siku 12—aliitaja diplomasia ya kielimu kuwa nyongeza na mkamilisho wa nguvu laini ya mfumo wa Kiislamu, na akasema: sharti la kusonga kuelekea ustaarabu mpya wa Kiislamu na ujenzi wa Umma katika ulimwengu wa Kiislamu ni kwamba; viashiria vyote vya nguvu na maendeleo, ikiwemo maendeleo ya kielimu na kiteknolojia, vifanyiwe kazi kwa pamoja kwa ajili ya kuiinua Iran katika medani ya kimataifa.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husseini Kouhsari alieleza kuwa kufanyiwa kazi diplomasia ya kielimu kunategemea utambuzi wa umuhimu na ulazima wake, pamoja na ujenzi wa mijadala na utamaduni katika uwanja huu kama moja ya mikakati mikuu katika taasisi za vyuo vikuu na hawza. Aidha, alitaja hali na mabadiliko ya dunia ya leo katika nyanja za teknolojia na mawasiliano, mabadiliko katika mahusiano ya kisiasa na ya ustaarabu, kujitokeza kwa nguvu mpya za kimataifa na kikanda, pamoja na migogoro inayotokana na ustaarabu wa kimada wa Magharibi, kuwa ni mazingira ya kihistoria ya kushangaza na yenye fursa kubwa kwa diplomasia ya kielimu ya nchi Iran.
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza za Kielimu alizitaja taasisi za kielimu kuwa na uwezo wa kipekee katika kufanikisha diplomasia ya kielimu, na akarejea uwezo kama vile uandishi na uchapishaji wa maelfu ya vitabu na kazi bora za kielimu, kuchapishwa kwa mamia ya majarida ya kisayansi na utafiti, uvumbuzi na ubunifu wa kisayansi katika taaluma mbalimbali, mbuga kadhaa za sayansi na teknolojia, maelfu ya vituo vya ukuaji na ubunifu, makongamano na matukio makubwa ya kielimu, uandishi wa nyaraka za juu za kimkakati, pamoja na uwepo wa mamia ya maelfu ya walimu na watafiti na mamilioni ya wanafunzi na wahitimu wa vyuo vikuu na hawza.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Husseini Kouhsari alitaja vipengele muhimu zaidi vinavyoathiri diplomasia ya kielimu kuwa ni: kujiamini kitaifa katika nyanja za sayansi na teknolojia, mjadala wa kibinadamu, Kiislamu na wa ustaarabu wa Jamhuri ya Kiislamu, nguvu laini ya Uislamu halisi na maarifa ya juu, uzoefu wenye mafanikio wa Jamhuri ya Kiislamu katika kufikia maendeleo ya kisayansi katika mazingira magumu zaidi ya vikwazo na mashinikizo mbalimbali ya mfumo wa ubeberu, pamoja na uwezo wa kuhamasisha nchi za eneo, ulimwengu wa Kiislamu na medani ya kimataifa. Alisisitiza kuwa Iran, kwa baraka ya Uislamu na maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s.), ndiyo kitovu pekee cha kielimu, na utafiti duniani chenye uwezo wa kushindana kiustaarabu na ustaarabu wa Magharibi katika nyanja zote.
Naibu wa Masuala ya Kimataifa wa Hawza alirejea baadhi ya vipaumbele katika kuhuisha diplomasia ya kielimu, vikiwemo: kuzingatia wanafunzi na maulamaa wasio Wairani wanaoishi Iran, kuipa kipaumbele miingiliano ya kielimu na wanaozungumza Kiajemi na Wairani wanaoishi nje ya nchi, kuzingatia miingiliano ya kielimu na nchi jirani na mhimili wa mapambano, kujali soko la pamoja la kielimu la ulimwengu wa Kiislamu, kutumia uwezo wa akili bandia, kupanua vikao na semina za kielimu za mtandaoni, kuunda vyama vya pamoja vya kielimu katika taaluma mbalimbali, kukuza safari na mabadilishano ya kielimu, pamoja na kutambulisha uwezo na mafanikio ya kisayansi na kiteknolojia ya Jamhuri ya Kiislamu. Aliongeza kuwa kufikia baadhi ya ngazi na tabaka za diplomasia ya kielimu ni rahisi na kunawezekana, na akasema: utekelezaji sahihi wa diplomasia ya kielimu unahitaji uratibu na ushirikiano na aina nyingine za diplomasia, ikiwemo diplomasia rasmi, diplomasia ya vyombo vya habari, diplomasia ya kitamaduni, diplomasia ya madhehebu na dini, pamoja na diplomasia ya kiuchumi.
Maoni yako